Posted on September 12, 2020 in Athletics, Media

Karibuni MT HANANG MARATHON 2020

Ndg wadau wa Michezo, taasisi ya GIDABUDAY SPORTS TOURISM FOUNDATION yenye ofisi zake Arusha inapenda kuwatangazia wadau kwamba Jumapili ya Septemba 27/2020 kutakuwa na mashindano ya MT HANANG MARATHON mjini Katesh Hanang.

Marathon ni mbio ndefu ya hadi Kilomita 42 lakini distance yoyote inayokimbiwa barabarani ambayo ni chini ya 42Km ni “MINI MARATHON” hivyo Katesh tutashirikisha Kilomita 10 na 5 kwa wakimbiaji au watakaopenda kutembea.

Madhumuni ya Bonanza hilo;

1)Kusaka vipaji vipya Wilayani Hanang na Mkoa wa Manyara kwa ujumla
2)Kuhamasisha amani kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020
3)Kuutambulisha umma mpango mkakati wa ujenzi wa uwanja wa kisasa Hanang
4)Pia tutaandaa semina ya siku moja (26/09) ya waalimu wa Michezo wa shule za msingi na sekondari (Sports General Knowledge for Beginners) ambapo vyeti vitatolewa

Ada ya kiingilio (registration fee) ni 15,000/ kupata namba ya ushiriki (Bib Number). Medali zitatolewa kwa washiriki wote (isipokuwa wanafunzi ambao watashiriki burr)), pia kutakuwa na zawadi za pesa taslim kwa washindi watano kwa wanaume na wanawake Kilomita 10, (zawadi zitatangazwa baadae).

Wanafunzi wa shule za msingi watashiriki bure (hakuna usajili) washindi 10 wavulana na 10 wasichana watapata vifaa vya masomo (schooling necessities).

Nyote mnakaribishwa….

Bib Number


Leave a Reply